Wednesday 19 February 2025 - 16:08
Usiweke kikomo maarifa kwa dhana za kiakili

Mjumbe wa Baraza Kuu la Seminari akisisitiza kwamba ujuzi haupaswi kutegemea dhana za kiakili pekee, alisema: Kujijua (kujitambua) si jambo la mtu binafsi tu, bali pia ni msingi wa kujenga jamii ya kimungu na inayoamini Mwenyezi Mungu mmoja. 

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Hawza, katika somo la maadili la Ayatollah Mahmoud Rajabi, Mjumbe wa Baraza Kuu la Seminari za Kitheolojia, mada ya "kujitambua na nafasi yake katika kumjua Mwenyezi Mungu na kupata furaha" ilijadiliwa.

Mjumbe huyo wa Baraza Kuu la Seminari amesisitiza kuwa, elimu binafsi si suala la mtu binafsi pekee, bali pia ni msingi wa kujenga jamii ya Mwenyezi Mungu na Tauhidi akitaja Aya na Hadithi za Qur'an.

Mjumbe wa Baraza Kuu la Seminari, akinukuu Aya za Qur'an na Hadithi za Utume (s.a.w.w), alisisitiza kuwa elimu ya kujitambulia si suala la mtu binafsi tu, bali ni msingi muhimu wa kujenga jamii ya Mwenyezi Mungu inayoamini Mwenyezi Mungu mmoja (Tauhidi).

Kujijua (kujitambua); Hatua ya kwanza kuelekea kwenye njia ya ukamilifu

Ayatollah Rajabi ameashiria kwamba watu mara nyingi hufanya makosa katika kujijua (kujitambua) wao wenyewe, na kutojua huko (ujahili huo) kunaziweka nafsi zao mbali na njia sahihi ya maisha.

Alinukuu maneno ya Amirul-Mu'minin Ali (a.s.):

"مَن لَم یَعرِفْ نَفسَهُ بَعُدَ عَن سَبیلِ النَّجاةِ ، وخَبَطَ فی الضَّلالِ والجَهالاتِ"

Asiyejijua (asiyejitambua), anapotea njia ya wokovu na anatembea katika bonde la upotofu na ujinga. Sentensi hii inaonyesha kwamba kujijua (kujitambua) si jambo muhimu tu, bali pia ni hitaji lisiloepukika katika njia ya ukamilifu wa Mwanadamu.

Mjumbe huyo wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi aliongeza: Kujijua kunamkomboa mtu kutoka kwenye mtego wa umimi na ubinafsi na kumpeleka kwenye unyenyekevu. Ikiwa ujuzi huu utakuwa imani ya moyo, itabadilisha maisha ya Mwanadamu.

Maarifa ya kujitamba kinafsi na maarifa ya Mwenyezi Mungu; Mabawa mawili ya kuruka kwa furaha

Aliongeza zaidi: Kujijua (Kujitambua kinafsi) na Maarifa ya kumjua Mwenyezi Mungu ni mambo mawili yasiyotenganishwa. Ikiwa Mwanadamu atajijua na kujitambua mwenyewe, hakika atamjua na kumfahamu Mwenyezi Mungu. Kwa maneno ya Imam Baqir (a.s): Hakuna maarifa yaliyo sawa na Maarifa ya Mwanadamu juu nafsi yake mwenyewe.

Maarifa haya ya kujitambua yanamfanya Mwanadamu kuelewa kwamba kila kitu katika ulimwengu huu kinamtegemea Mwenyezi Mungu na hakuna kiumbe anayejitegemea yeye mwenyewe. Imani hii inamzuia mtu kutomtilia maanani asiyekuwa Mwenyezi Mungu na kumpeleka kwenye Tauhidi ya kweli.

Ayatollah Rajabi, akirejea hotuba ya Allamah Tabatabaei (RA) kwamba “Kutoijua nafsi yako ni mwanzo wa maovu yote ya kimaadili”, amesema: Kinyume na ujinga huu, kujijua nafsi yako na na kumjua Mwenyezi Mungu humkomboa Mwanadamu kutokana na umimi na ubinafsi na kumpeleka kwenye imani, shukrani na utiifu wa kweli kwa Mwenyezi Mungu.

Kujijua - Kujitambua - na Jukumu lake katika Jamii

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake ameashiria nafasi ya kujitambua katika jamii na kusisitiza kuwa iwapo watu watajitambua nafsi zao wenyewe, jamii nayo itaelekea kwenye wema na furaha. Jamii ambayo watu wake hawajitambui itakabiliwa na kila aina ya matatizo ya kimaadili na kijamii.Kujitambua huku sio tu kwamba kunamboresha mtu binafsi, lakini pia kuna athari chanya kwa jamii nzima. Jamii yenye misingi ya kujijuana kujitambua na kuamini Mwenyezi Mungu mmoja, itakuwa mbali na uonevu, ufisadi na ukosefu wa haki na usawa.

Kujijua - Kujitambua - na kuamini Mwenyezi Mungu mmoja kwa vitendo

Mjumbe huyo wa Baraza la Wataalamu wa Uongozi alidokeza kuwa kujijua (kujitambua) na kuamini Mwenyezi Mungu mmoja hakuishii katika nadharia na fikra tu, bali lazima pia kudhihirika kivitendo. Ikiwa mtu anaamini kwamba kila kitu kinatoka kwa Mwenyezi Mungu, basi kwa vitendo anamwamini tu Mwenyezi Mungu na hatafuti msaada kutoka kwa mwingine yeyote yule asiyekuwa Mwenyezi Mungu.

Mwishoni, Ayatollah Rajabi alisema: Sote tunapaswa kujitahidi kujijua (kujitambua) sisi wenyewe nafsi zetu na kumjua na kumtambua Mwenyezi Mungu, na tusiiwekee elimu hii (na maarifa haya) mipaka ya kwenye dhana za kiakili tu, bali tuigeuze kuwa imani ya moyo, ni hapo tu ndipo mtu atakapoweza kupata furaha ya kweli na kuachiliwa kutoka kwenye mtego wa ujinga (ujahili) na udanganyifu.

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha